Jambo kwa wote, mimi ni Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.
Moja ya ujuzi wa muhimu kwa msimamizi wa upandaji wa makanisa ni uwezo wa kusimulia hadisi ya Mungu kwa uwazi, kwa ufupi na kwa kushawishi. Biblia inatuhadisia hadisi kubwa. Lakini Biblia ni kubwa. Siyo Kitabu kimoja, lakini ni mchanganyiko wa vitabu 66 tofauti ambavyo vinaambatana vyote kuelekea Yesu, Mwokozi wa ulimwengu. Hivo basi, wakati tunapotangaza injili, tunapo fundisha, tunapo omba, ao kushauri, tunastahili kuchunga moyoni hadisi kubwa na kuirejelea mara kwa mara.
Kwa mda wa myezi tatu ya mpango mpya wa upandaji wa makanisa katika vijiji, wasimamizi wa upandaji wa makanisa wanajifunza kusimulia hadisi ya Mungu mnamo dakika 10 ao chini ya mda huo. Bali, ili kuweza kufupisha kiini cha neno la Mungu kwa hadisi ya dakika 10, inastahili kuifahamu vizuri. Kwa kweli, inastahili kujuwa hadisi ya kila kitabu cha Biblia na kuelewa Mada zake maalum, kama vile upendo, utakaso na dhambi, kujitolea na wokovu, ukombozi na msamaha, pamoja na neema na imani. Lakini usivunjike moyo kama haujuwe vizuri vitabu vyote vya Biblia wala kama hauelewi vizuri Mada zake maalum. Anza kusimulia hadisi kubwa ya Mungu ukifuata mtindo wa miviringo tatu. Daima ongeza ufahamu wako kuhusu hadisi hii. Soma ao usikie Biblia katika lugha yako ya asili. Anza kusoma Mwanzo na umalize na Ufunuo. Usiogope kama hauelewi vipendele vyote. zingatia tu mada maalum za Biblia.
Kwa kuendelea kwako kusoma, Mada hizi zitajirudilia bila kukoma : upendo na msamaha, utakaso na dhambi, kujitowa na wokovu, ukombozi na msamaha, pamoja na neema na imani.
Zaidi unavyojuwa watu muhimu na Mada za muhimu za Biblia, zaidi utatayarishwa kusimulia hadisi ya Mungu kwa ufupi na kwa ukubalifu.
Inastahili kujuwa kila kifungu cha Biblia ili kutangaza hadisi ya Mungu kwa misheni ya injili wala mafundisho kwa wanafunzi ?
Apana. Lakini zaidi unavyoelewa, vizuri zaidi utaweza kusimulia hadisi ya Mungu na kuikabili sawasawa na maitaji ya wasikilizaji . Stafano, moja ya watu wa Mungu walio na ushawishi zaidi, aliishi pamoja naye. Hadisi yake inasimuliwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, sura ya 7. Stafano alijuwa hadisi ya Mungu. Alipoalikwa, alijuwa kuisimulia kwa ufupi na kuweka mojamoja kwenye vitendo. Hata kama wasikilizaji wake hawakuitikia vizuri, ushuhuda wake uliashiria mabadiliko katika historia ya kanisa.
Utukufu wa Mungu ulijitukuza wakati Stefano alisimulia hadisi yake kwa ujasiri. Sasa, usivunjike moyo na uendelee na utafiti wako ili kujuwa hadisi ya Mungu, kwa kuelewa Mada maalum na kujuwa kuisimulia. Kama hauna Biblia ya sauti katika lugha yako ya asili, jielekeze kwenye mtandao wa Google Play store ili uweze kupokea (télécharger l'application Bible) na hapo utapokea Biblia za sauti katika ma mia za lugha za nyumbani.
Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi Dean Davis, nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni