Jumatano, 15 Aprili 2026

Maendeleo ya Uongozi - Baazi ya tabia za ziada za kutafuta kwa viongozi wanaojitokeza

 












Mimi ni Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wasimamizi na wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Mada yetu katika mwaka huu wa 2026 ni maendeleo ya Uongozi. Katika vipindi vyangu viwili vya nyuma, niliongea kuhusu tabia mbali mbali ambazo nazitafuta kwa viongozi wanaokuja. Kwa mtazamo wangu, cha muhimu ni utambulisho mkubwa unao shikamana na Yesu-Kristo pamoja na unyenyekevu. Turu ya mwisho niligusia

umuhimu wa historia na ujuzi wa mtu.

Leo, natarajia kugawanya mawazo mamoja kuhusu tabia zingine tatu ninazo zitafuta kwa viongozi wanaokuja : mpangilio, hamu ya kufunzwa na kukomaa, usikivu wa kupokea mafundisho.

Nafikiri kwamba munaweza kuona ukamilishano wao.

* Mpangilio unatafsiriwa kama "uwezo wa kuchunguza na kuanzisha vitendo kwa namna ya kibinafsi". Walio  na moyo wa kuongoza hawangojee kuambiwa nini watafanya. Wanatenda. Isipokuwa, kitu cha muhimu ni kwamba wafanye yaliyo "haki", na ndipo hapo uchunguzi unakuwa wa muhimu. Kwa kurudilia podikasti yangu ya nyuma, mtu iko na tabia ya kufanya uchunguzi wa haki na kutenda ipasavyo? Nafikiria watoto wa Isakari katika 1Mambo ya nyakati 12:32. 

"Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao."

* Ya pili, hamu kubwa ya kujifunza na kuendelea ni muhimu kwa maendeleo ya viongozi wanaokuja. Mara nyingi wanasema ''viongozi ni wanafunzi" na ninaamini kama ni kweli kabisa. Wakati ninapochunguza viongozi wanaokuja, ninakuwa mwangalifu kwa wale walio na moyo wa kupenda kujuwa na wanaoitaji kujifunza elimu mpya na kuendeleza ujuzi mpya. Hawasite kutowa nguvu na mda mwafaka ajili ya kuendelea,  katika suala la nguvu na uwezo.

* Kwa kulinganisha moja kwa moja na nukta yangu ya pili, ni muhimu kwamba viongozi wapya wawe wasikivu kwa mafundisho. Mithali 1:5 inatushauri "mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.'' viongozi vijana wanastahili kuonyesha alama ya unyenyekevu (kama nilivyoizungumzia mwezi uliyopita) kwa kusikiliza na kujifunza, na wanastahili kuwa wenye utambuzi kwa mashauri wanayopokea. Wakati ninapo tazama na kuchunguza viongozi wapya, ninatafuta kutambuwa  washauri wao. Je ! Wako na mwenendo mzuri wa kufuata?

Nitaendeleza mawazo yangu kuhusu tabia za kutafutwa kwa viongozi wanaokuja katika podikasti yangu inayokuja.

Ujumbe huu ni wa kutiya moyo kwa wapandaji na wasimamizi wa makanisa katika vijiji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...