Ijumaa, 11 Septemba 2026

Umpende Jirani yako

 











Jambo kwa wote ! Naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Amri ya Yesu inayotufundisha kumpenda Jirani kama nafsi zetu wenyewe inaonekana kama vile ni ya kawaida kama vile mimi, ulikomaa ukienda kanisani, ukishiriki darasa za watoto na vijana. Lakini, kama vile mambo mengi yaliyoyafundishwa na Yesu, amri ya kumpenda Jirani kama nafsi zetu wenyewe hakika ni amri isiyo geuka. Kwa kuelewa ni kwa kiasi gani amri hii ni shurti, tukumbuke hadisi ambayo Yesu alisimulia kwa kusaidia mtu aliyejidai kuwa mwenye haki kwa macho yake mwenyewe akielewa nini inayo maanisha Kumpenda Jirani.

"Luka 10:30-35

[30]Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa. 

[31]Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.

[32]Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando. 

[33]Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia, 

[34]akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza. 

[35]Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa."

Hadisi hii inatufundisha kwamba Jirani zetu siyo wale tu wanaoishi kandokando yetu na wanaotujuwa vizuri. Tunaitwa kuwapenda wageni, kama Msamaria alivyofanya.

Hadisi ya Yesu inatufundisha kama upendo zidi ya Jirani yetu itazuiya miradi yetu.

Kumpenda Jirani yetu pia inagharama. Kama tunatarajia kupenda wengine, tunastahili kuwa na moyo mwema.

Kwa mwisho, tunajifunza kupitiya hadisi ya Yesu kama kumpenda Jirani yetu inamaanisha kuwapenda watu wasiokuwa wa kabila letu ao wa taifa letu, kama Msamaria alivyopenda huyu mtu Myahudi aliyepigwa.

Upendo ambao Yesu anatuamuru siyo wa jinsia ao ule wa hisia. Siyo pia upendo wa faida ambao Yesu anatuomba kuonyesha. Siyo rahisi kutii amri ya Yesu ya kupenda Jirani kama sisi wenyewe.

Upendo ambao Yesu anatarajia kwetu zidi ya Jirani zetu hautokani tu na hali yetu ya utashi tukiwa kama wanamemba wa jamaa wala ukoo. Yesu anatuita kumpenda Jirani yetu kwa upendo wa kujitolea.

Hii inaweza kuwa tatizo kubwa kwa waamini wapya, zaidi kama walikuja kwa Yesu wakitumainia kwamba Yesu atatatuwa shida zao. Ni kweli Yesu anajibia maitaji yetu mengi katika dunia hii, na shida zetu katika dunia ijayo.

Lakini pia anaitaji kuona tukionyesha tabia yake, huruma yake na neema yake.

Anatarajia kuona tunawapenda Jirani zetu kwa upendo wa kujitolea.

Ijapokuwa, siyo rahisi kutii amri zote za Yesu. Tunaitaji nguvu yake, uwepo wake na upendo wake hata akitumika ndani yetu.

Sasa, muwafundishe vizuri wanafunzi wenu ukuu wa upendo wakujitolea wa Kristo.

Muwafundishe kama hatawaacha kamwe yatima.

Lakini pia muzidi sana kuwafundisha kuweka tumaini lao kwa Kristo ili kupokea uwezo unaostahili kuwapenda Jirani zao kama wenyewe.

Ilikuwa "Ongezeka". Mimi ni Dean Davis, nawauliza swali hili : "Ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Maendeleo ya Uongozi - Yesu anafundisha makutano na kutowa maelekezo kwa Mitume

    Mimi ni Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na viongozi wakikristo katika vijij...