Jambo kwa wote, Naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.
Kwa siku hizi za mwisho, ndani ya vipindi hivi, tulichambuwa mada zinazo ambatana na Mada ya ongezeka. Tulikumbusha kwamba njia moja tu ya kutekeleza maoni ya VCP - kanisa moja katika kila Kijiji cha Afika ifikapo mwaka wa 2050 - ni kwa njia ya ongezeka.
Sababu tunapenda Mungu na tunataka kutekeleza Agizo kubwa ya kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi na kwa mahali pote. Tunayo imani katika ongezeka. Roho ya upandaji wa makanisa katika vijiji, VCP ni ongezeko la wanafunzi, waviongozi na makanisa.
Kama tunapendelea kuongeza wanafunzi na viongozi, tunastahili kufanya vizuri zaidi tu ya kuwafundisha mawazo mapya. Tunastahili kuwapa fursa ya kutenda. Kutowa namna, ni kupana nguvu, uwezo na mamlaka. Viongozi wa kikristo wenye busara wanajuwa kama kuko namna nyingi ya kufikia hapo.
Tunatowa uwezo kwa wengine kwa kuwashauri (kuwafundisha) kupitiya mashauri na kwa kuwakilisha majukumu na mamlaka.
Namna ingine ya muhimu ya kuwaacha wengine huru ni mafundisho. Yesu alitowa uwezo kwa wanafunzi wake kwa kuwafundisha : aliwafundisha Ufalme wa Mungu, na kufanya huduma kwa wengine.
Lakini, kwa bahati mbaya, mafundisho yote hayana ndani yake uwezo. Watu wamoja wanafundisha tu sababu wanapendelea kusikilizwa wakisema mawazo ya muhimu.
Wengine wanafundisha sababu wanapenda kupata heshima inayopewa Mwalimu. Wengine wanafundisha sababu wanafurahia vile watu wanakaa kimya wakiwasikiliza. Alafu, waalimu wanaofundisha kwa lengo la kusifiwa ao kuheshimika mara nyingi hawatowe sana uwezo kwa wanafunzi wao.
Sasa, ni hatuwa ao tabia gani za waalimu wanaotowa uwezo kwa wengine?
Namna Mwalimu anastahili kufundisha wakati anatarajia kudumisha na kuwafanya wanafunzi wake wawe na ujuzi wa kuongoza? Huduma ya Yesu inatupatiya jibu nzuri kwa swali hili. Mafundisho ya Yesu yalijaa huruma. Mafundisho yake hayakuwa rahisi kuyaelewa, sababu yalijaa utuwema.
Mathayo 4:23 inatuambia:
''Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu''
Yesu alionyesha huruma yake kwa kuchukuwa miaka tatu kwa kutayarisha wanafunzi wake kwa majukumu yaliyo makubwa zaidi. Aliwatuma wanafunzi wake kazini na kusikiliza ripoti zao wanaporudi. Yesu alionyesha tendo la uvumilivu kwa wanafunzi wake. Kamwe hakuwaacha wenyewe, hata wakati walikuwa na uzaifu wa kujifunza na kuelewa.
Je! Na weye? Wanafunzi wako wangekuonyesha wewe kama mtu aliye na uvumilivu na utuwema?
Wakati unapofundisha, unachukuwa mda wa kusikia? Wanafunzi wako wangesema kama unawapa mda na unatafuta kuwaelewa? Wanajuwa kama unawaaminia na unasubiri kuwaona wakitekeleza mambo makubwa? Mwalimu wako anajaa utuwema na huruma ?
Kama ni hivo, msifu Bwana na uendelee na kazi yako nzuri. Lakini ukijisikia kwamba ndani mwako unakosa huruma, chukuwa wakati leo hii kumwambia Bwana. Umwambiye kama unasikitika kwa ukosefu wako wa uvumilivu mbele ya wanafunzi wako na ukosefu wako wa utuwema.
Uwe mwangalifu. Omba kwa unyenyekevu kwa Bwana akujaze na huruma kwa wale unaowafundisha. Umwambiye kama unapendelea sana kuwapa namna ya kuishi kama wanafunzi.
Bwana atajibu kwa ombi lako, kama anavyosema Yakobo 4:6:
''Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.''
Mimi ni Dean Davis, nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni