Tazama Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutia moyo kwa wapandaji wa makanisa na viongozi wa Kikristo katika vijiji.
Leo, tunaendelea na mfululizo wetu wa uongozi wa uwakili. Mwandishi mmoja anafafanua muwakili kuwa "mtu anayesimamia rasilimali za mtu mwingine ili kufikia malengo ya menye mali."
Katika mazi'gira yetu, tunasimamia rasilimali zinazotolewa na Bwana kwa kazi yetu ya upandaji makanisa katika vijiji.
Mfano wa msimamizi dhalimu unapatikana katika Luka 16:1-13. Ninakuhimiza utulie na uisome. Kwa mtazamo wa kwanza, hadithi hii inaweza kuonekana kuwa ya kutatanisha. Kwa nini bwana wa nyumba angemsifu msimamizi-nyumba asiye mwadilifu kwa kutenda kwa busara? (Tutashugulikia swali hili katika sehemu yangu inayofuata. Katika podikasti hii na mbili zifuatazo, tutachunguza mada tatu ninazoona katika hadithi hii:
- Wasimamizi lazima wawajibike.
- Utambuzi wa msimamizi na sifa kutoka kwa bwana wake.
- Umuhimu wa uaminifu katika mambo madogo na katika kusimamia fedha. Kwa kuanzia, nazani ni muhimu kwamba mfano huu unafuata mara moja ule wa mwana mpotevu aliyetapanya mali ya babake.
Ni lazima pia tufikirie mazi'gira ya fundisho hili:
Yesu anazungumza na wanafunzi wake na Mafarisayo, viongozi wa kidini wa wakati huo. (Tunaona hili mwanzoni mwa sura ya 15.Tunasoma yafuatayo katika sura ya 16, mstari wa 1 na 2 : “Palikuwa na mtu mmoja tajiri ambaye msimamizi wake alishitakiwa kwa kutapanya mali yake. Anamtolea hesabu msimamizi wa nyumba asiye mwadilifu ambaye aliona mali za bwana wake kuwa njia ya kujifurahisha na kujiletea maendeleo. Mstari wa 1 unasema "alipoteza" rasilimali za tajiri. Baadhi ya tafsiri zinasema "alizitapanya". Msingi ni kwamba Baba yetu anatuomba tuwe mawakili waaminifu.
Yesu anataka wafuasi wake wawe wasimamizi wa nyumba wenye haki na waadilifu. Hebu tuangalie tena wasikilizaji wa Yesu. Anawakemea kwa kutosimamia ipasavyo baraka na majukumu yanayowapata wakiwa wateule wa Mungu. Wasikilizaji wengine walikuwa wanafunzi wake (ona mstari wa 1), ambao sisi ni sehemu yao leo. Ikiwa tunaelewa kanuni kwamba kila kitu tulicho nacho ni zawadi kutoka kwa Mungu, tunatambua kwamba Mungu ndiye mmiliki wa vyote tulivyo tulivyo navyo, na kwamba sisi ni mawakili wake. Kwa hivyo, lazima tutumie rasilimali za Mwalimu kufikia malengo ya Mwalimu''.
Katika kipindi chetu cha kufuata, tutaendelea na somo letu kuhusu uongozi wa Muwakili, kwa kutafakari utambizi wake.
Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wa kikristo katika vijiji.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni