Jumanne, 10 Juni 2025

UONGOZI WA MUWAKILI - Mfano wa Talanta - Sehemu ya 3



Tazama Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo katika vijiji.

Kwa mwanzo huu wa mwaka, nilianzisha mtiririko mpya kuhusu Mada ya uongozi wa Mawakili.

Mwandishi moja anatafsiri Mwakili kama ''mtu anaye ongoza rasilimali alizopewa na mtu mwengine ili kufikia malengo za mwenye mali''.

Leo, tunaendelea mafunzo yetu ya mfano wa Talanta, unaopatikana katika Mathayo 25 :14-30.

Katika vipindi viwili vilivyopita, tulijifunza kanuni saba ambazo zilitolewa katika hadisi hiyo.

Ningependelea kufafanuwa mambo mamoja ambayo hatuoni katika mfano huo wa Yesu.

Kwa kuanza, napendelea kuwapasha alama moja ya muhimu saana.

Wasimamizi Mawakili wanaongoza kwa unyenyekevu.

Tazama baadhi ya maoni ambayo hatuyaoini kwa Mwakili aliye tangulia na Talanta 5 na akamaliza na Talanta 11.

- hakumuamakia wala kumutukana Mtumishi aliye tumika vibaya na Talanta yake moja. Mwakili ''mwaminifu'' alimwachia mwenye mali hatua ya kumtangaza ''mbaya, mvivu na asiye na maana''. Kama wanadamu, mara nyingi tunajaribiwa kwa kuhukumu wengine, na tunastahili kuwa waangalifu kwa jambo hilo. Tunastahili kumwachia Mungu na wale wenye madaraka kujihusisha na Wale wasiojibu kwa ukamilifu kwa yanayotarajiwa.

- jambo la pili, hatukuona Mtumishi aliye na Talanta 11 kufurahia yule aliye na 4. Pengine utakumbuka kama nilivyosema katika podikasti yangu ya nyuma, Mtumishi aliye pokea mifuko tano na ule aliyepokea mifuko mbili walisifiwa sawasawa na bwana wao. Ni vema, Mtumishi mwema na mwaminifu kwa mambo madogo ; nitakupa vitu vingi. Njoo tuchangia mema ya bwana wako. Nakazia tena unastahili kuepuka mtego wa kujilinganisha na wengine.

- kwa mwisho, nafurahia Mtumishi aliye na Talanta 10. Siyo mda wa kujisifia (tunayaona mara nyingi kwa wajezaji) kwa kujihusisha na umimi. Chukulia hii mifano ya Yesu katika Luka 17:10. ''Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya''. 

Hakuna nafasi ya kujiinuwa ndani ya mifano hii ya Yesu.

Hata kama Mtumishi aliye maliza na Talanta 11 alisifiwa na mwenye mali, alibaki tu Mtumishi.

Sisi kama wasimamizi Mawakili, tunapashwa kuonyesha mwenendo wa upole, kwa kutekeleza kila siku kwamba yote tuliyo nayo, na vyote tulivyo, ni vya mwenye mali, Bwana Yesu-Kristo.

Katika toleo letu la kufuata, tutaendelea na mafunzo yetu kuhusu uongozi wa Mawakili.

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo katika vijiji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...