Jumatano, 13 Novemba 2024

Uvumilivu - Siku 90 za Maombi na Kufunga


 





Jambo kwa wote, hii ni Ongezeka, podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa , na viongozi wa Kikristo katika vijiji. Mimi ni Brad Snowden, na kwenye podikasti hii. Nataka kukuhimiza uvumilie. Tumebarikiwa sana kwamba Bwana ametupa kila mmoja wetu zana zenye nguvu ambazo tunaweza kukua, ni kwa neema ya Mungu kwamba ametupa neno lake ambalo tunaweza kuona moyo wake. Anatamani kila moyo umjue na kuujua upendo wake, kuna wakati lazima tuinuke vitani tukiwa na moyo wa shujaa ili tuone na kujionea ushindi, ushindi mkubwa ni kumuona Yesu akibadilisha maisha na tunapoomba tuwe mashujaa wa kudumu. , Waefeso 6:10-18 mtume Paulo anatupa ufahamu wa silaha za Mungu na chombo cha mwisho ni maombi, Waefeso 6:18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati, kila nyakati na nyakati zote katika roho. Mukeshe kwa ustahimilivu wote na kuomba maombezi katika maombi kwa ajili ya watu wote wa Mungu naamini hili si wazo la mwisho au wazo la ziada, bali ni chombo chenye kuunganisha silaha zote pamoja ili kuwa na ufanisi kwa mioyo ya wale ambao bado hawajampokea Yesu. Ee kanisa, Mpandaji, kiongozi, kaka na dada, na tuinuke katika uweza wa uweza wake, tuwe tunasimama, kupiga magoti, au kutembea, ni maombezi ya kudumu kwa niaba ya wengine ambao Mungu ataheshimu.

Hii haimaanishi kwamba itakuwa rahisi, mbali na hayo, lakini kuvumilia ni kuendelea kutembea kana kwamba hakuna kitu kinachotuzuia. Bwana ataheshimu uvumilivu wetu tunaposonga mbele katika matembezi yetu pamoja Naye. Usichoke, bali mruhusu Mungu akuimarishe katika mwendo wako wa kudumu na katika maombezi yako kwa niaba ya wengine. Ninaomba kwamba kila mwamini Yesu awe mwombezi mkuu wa mioyo katika kila kijiji barani Afrika. Tutapata ushuhuda wa uaminifu wa Mungu tunapomwita kwa uvumilivu. Ilikuwa neno la kutia moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji. Ni Nani utakayemshirikisha hii leo, Bwana akubariki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...