Alhamisi, 10 Oktoba 2024

Watiye Moyo Waombezi Wako - Siku 90 za Maombi na Kufunga


 Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Sote tunaitaji waombaji. Tunaitaji sote watu wanaokuwa kati yetu na Mungu na wanaotuombea. Maombezi, ni kuingilia kati kwa niaba ya mtu mwingine. Maombi ya maombezi ni maombi yanayoelekezwa kwa Mungu kwa faida ya watu wengine. Kama wapandaji wa makanisa, munaitaji maombi kwa mda wa siku 90, ao zaidi ya mda mwengine wote tangia pale ulipo anza kupanda makanisa.

Unaitaji kuomba ili mbingu zifunguke. Unaitaji waombaji ili kumsihi Mungu kueneza Roho wake kwa kuwavuta wanaume na wanawake kwake,  wakati wewe na wanafunzi wako munagawanya Habari Njema.

Unaitaji maombi ili milango ifunguke,  wakati wewe unawatafuta wanaume na wanawake wa amani katika vijiji ambako bado hakujakuwa makanisa. Na unaitaji maombi kwa ajili ya ukingo wa kimwili na kiroho wakati wewe pamoja na wanafunzi wako munatangaza Habari Njema.

Kama mujuavyo kupitiya maombi yenu na kifungo, maombezi ni kazi ngumu.

Kwanza, unaitaji kuwa na mda.

Na ni kweli, inaitaji imani.

Waombezi wanastahili ku amini kwamba  Mungu iko na anawalipa wale wanaomtafuta kwa bidii (Waebrania 11:6).  Lakini kuko mtindo mwengine wa maombezi unaotuchokesha. Maombezi ni kazi ngumu sababu tunapambana ndani ya maombi. Tunapambana zidi ya adui anayeonekana kushinda mapambano kwa maeneo mengi. Na tunapambana zidi ya mashaka yetu.

Inachokesha. Kwa hiyo, hata waombezi wenye uzoefu wanajaribiwa kutokuomba zaidi. Waombezi wote wanaitaji kutiwa moyo.

Kwa hiyo, ni namna gani kuwatiya waombezi moyo ? Mbele ya yote, tunawakumbusha wema wa Mungu. Tunagawanya ushuhuda wa maombi yaliyo jibiwa. Kusikia namna gani Mungu mwema na mwenye upendo alivyo jibia maombi yao na yetu inasisimuwa imani kwa ajili ya maombi mengi.

Ya pili, tunawakumbusha ahadi za Mungu kwa kusikia na kutekeleza maombi yetu. Kuko ahadi nyingi katika Agano la kale na jipya.

Lakini moja ya ahadi hizo inayo nijenga katika maombi yangu inapatikana katika 1Yohana 5:14;15 :

''Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 

Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.''

Wakati tunapo omba kwa ajili ya waliopotea na kwa ajili ya makanisa mapya, tunajuwa kwamba tunaomba kulingana na mapenzi ya Mungu.

Kutiwa moyo kwa namna gani !

Namna ya tatu ya kuwatiya moyo waombezi ni kugawanya pamoja nao maitaji mapya ya maombi maalmu.

Na namna ya ine ni kuwashukuru tu kwa ajili ya kazi kubwa ya maombi ambayo wamejitolea.

Mpandaji mpenzi wa makanisa, unaitaji waombezi na waombezi wako wanaitaji kutiwa moyo, zaidi kwa mda wa Siku 90 za maombi, kifungo na upandaji wa makanisa. Unapendelea kuimarisha imani yao kwa Neno la kutiya moyo leo ?

Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi Dean Davis nawashukuru kwa ajili ya uaminifu wa maombezi yenu kwangu zaidi ya wapandaji wa makanisa katika vijiji 13 000 kwa Afrika .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...