Jambo, tazama ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa, wachungaji na viongozi wa Kikristo. Mimi ni mgeni wenu Daneille Snowden.
Andiko linatuimiza kuombeana, Sisi kama viongozi wa Kikristo wa kanisa la Yesu-Kristo, ni muhimu sana kuombea wale wanaotumika kwa ajili ya ufalme wa Mungu.
Ninapenda hii andiko : Wakolosai 4:2 : lisemalo ''Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani;
mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa,''
Kuomba kuko na tafsiri ya kushangaza kwa kutenda kwa kila hatuwa ya maisha yetu.
Kwa kuomba, tunastahili kuwa wanyenyekevu ndani ya roho yetu, tukimwomba Mungu kwa utaratibu mkubwa.
Hiyo inaungana na tendo lakuendelea, kwa hiyo, ''kuomba'' na kuendelea kuomba ! Kwa mwisho tunaomba bila kukoma.
Sisi kama wapandaji wa makanisa na viongozi wa makanisa, wakati tunapo omba kwa ajili ya watumishi wetu wote, tunaomba kama vile Paulo alivyofundisha katika Wakolosai :''... Ili kwamba Mungu afungue mlango kwa ujumbe wetu, ili kwamba tutangaze maajabu ya Kristo...''
Tuendelee kuombea watumishi na sisi wenyewe ili kwamba'' ...Injili hii ya Ufalme itangazwe duniani mzima kama ushuhuda kwa mataifa yote, na baadaye mwisho utatokea ! Mathayo 24:14
Hiyo ilikuwa ongezeka, munaweza tafazali kuigawanya na wengine?
Asante na Mungu awabariki.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni