Jumatano, 20 Novemba 2024

UMPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO MWENYEWE




    Jambo kwa wote,  naitwa Dean Davis na tazama "Ongezeka", ni podikasti inayoleta neno la kutia moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji. 

Moyo wa Injili ni upendo. Kwa sababu ya upendo wake mkuu, Mungu alimtuma Mwanawe ulimwenguni kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. Mungu anaonyesha upendo wake kwetu kwa kumfanya Kristo afe kwa ajili yetu tulipokuwa tungali wenye dhambi. Moyo wa Injili ni upendo. Mungu ni upendo. Na kwa sababu Mungu ni upendo, amri kuu ni kumpenda Mungu na ya pili inafanana: kumpenda jirani kama sisi wenyewe. Maandiko yanaonyesha waziwazi kwamba kumpenda jirani kunamaanisha kujitolea ili kuwasaidia kwa njia inayofaa. 

Yesu alisimulia hadithi ya Msamaria Mwema ili kuonyesha ukweli huu. Msamaria alipomwona yule mtu njiani kuelekea Yeriko aliyekuwa amepigwa na wezi, alisimama, akamtunza, na kumfunga vidonda vyake. Hata alilipia na pesa yake katika hoteli hiyo. Upendo ni vitendo. Ikiwa upendo haufanyiki, sio kitu. Lakini upendo pia ni wa kiroho. Mungu anaonyesha upendo wake kwetu kwa kumtuma Mwanawe kufa msalabani ili dhambi zetu zipate kusamehewa. Mungu, kwa upendo wake, alimshinda Shetani kupitia kifo na ufufuo wa Yesu. 

Haya ni mambo halisi ya kiroho, lakini ni halisi sawa na hali halisi ya kivitendo ya kutunza mtu aliyejeruhiwa na kuteseka. Unaona, upendo wetu kwa jirani unatokana na upendo wetu kwa Mungu. Upendo wote hupata asili yake kwa Mungu, kwa sababu Mungu ni upendo.

Kwa sasa, haya yote yanamaanisha nini kwetu Sisi kama wapandaji wa makanisa ?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...