Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka''ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji. Mara ya mwisho nilipozungumza nawe, nilikuuliza swali. Nikauliza, “Unafanya nini unafikiri ni kifaa gani inayohitajika zaidi kwa ajili ya kuongeza makanisa? Majengo, pesa, sala, au watu? Ni wazi kwamba aina zote nne za rasilimali ni muhimu. Lakini ni zote zilizo muhimu kwa upandaji wa makanisa? Na hata ikiwa zote ni rasilimali muhimu, ni ipi kati ya hizo ine, majengo, pesa, maombi, au watu wengi iliyo ya muhimu?
Nadhani hakuna jibu la mwisho dhahiri kwa swali hili ambalo linafanya kazi ndani kila hali ya upandaji wa makanisa wakati wote. Lakini ningependa kusema kwamba kwa ujumla, watu ndio rasilimali ambayo huduma yako ya upandaji wa makanisa inahitajika zaidi kuliko yoyote nyingine. Lakini kufikiria watu kama rasilimali inaweza kuwa hatari kwa kiasi fulani. Watu wameumbwa kwa mfano wa Mungu. Watu wote wanastahili, utu, na heshima. Kwa hivyo, ikiwa tunafikiria watu kama rasilimali tu, tunaweza kuangukia majaribu ya kuwachukulia tu kama vyombo na zana za kufikia malengo yetu.
Hilo litakuwa kosa la dhambi. Lakini Kuna njia ya kuwafikiria kwa unyenyekevu watu kama rasilimali wanaomfikia Mungu- wamepewa malengo kwa ajili ya kanisa kufanya wanafunzi wa mataifa yote. Njia hii ya unyenyekevu kufikiri huanza kwa kumthamini kila mtu kwa hazina ya thamani aliyonayo, ni Mungu amekupa watu wengi wanaoabudu katika makanisa yako. Kiasi gani unajua kuwahusu?
Je! unajua hadithi zao kwa kiasi gani? Ni nini kinachochochea kila mmoja? Je, ni karama, ujuzi, na pesa gani wanaleta kwa makanisa yako? Jinsi gani vipawa vyao vinakuzwa na kufanyiwa kazi ili kuendeleza kazi ya Kristo? Sisi ni mawakili, yaani sisi ni wasimamizi wa rasilimali tunazopewa na Mungu. Ni wajibu wetu wa kusimamia rasilimali hizo vizuri. Jukumu moja la muwakili ni kuhakikisha rasilimali zake zinazalisha na kukua, si kupungua bila kutumika. Unaweza kukuza rasilimali watu wa makanisa yako kwa njia tatu:
Kwa kutoa maono
Kwa mafunzo na kufundisha
Kwa kuhamasisha karama za kiroho Njia hizi tatu za kuendeleza watu kama rasilimali zinakwenda pamoja. Unajua kuhusu kutoa maono ili kuwasaidia watu kuona mpango wa Mungu na mbinu za Mungu kufikia malengo yake. Unajua jinsi ya kuchora picha ya neno la kile ambacho Mungu ana mawazo na kuamsha imani.
Na unajua kuhusu mafunzo na kufundisha kutoa mpya kuelewa na kuwasaidia watu wako kukuza ujuzi mpya wa huduma. Uhamasishaji wa karama za kiroho hujengwa juu ya maono, mafunzo, na kufundisha. Uhamasishaji wa karama za kiroho unauliza maswali mawili:
1. Ni karama gani za kiroho ambazo Mungu amewapa watu ambao nimewafundisha? 2. Vipawa hivi vinawezaje kutumika kufikia malengo tuliyopewa na Mungu ya kuzidisha wanafunzi, vikundi vidogo vidogo, na makanisa
Viongozi wanaotaka kuongeza makanisa hujiuliza maswali haya kila mara. Kama Mungu hutoa majibu kupitia uchunguzi, maombi, na tafakari, viongozi kuwa mawakili wazuri wa rasilimali za watu ambao Mungu amewakabidhi. Kupitiya kwa njia hii wanaweza kuwawezesha wafanyakazi kutumikia Kanisa kadiri ya karama zao. Hii inasababisha matokeo makubwa zaidi ya Injili na sifa nyingi kwa Bwana.
Hii ilikuwa Ongezeka na mimi ni Dean Davis nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?
#Kuhamasisha Karama
#Rasilimali Watu

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni