Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji. Kufanyika mwili kwa Bwana wetu Yesu Kristo kumejaa ajabu na fumbo, nguvu na baraka. Ni furaha ya namna gani kwa hiyo kusherehekea Krismasi. Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu. Tumeuona utukufu wake, utukufu wa Mwana pekee aliyetoka kwa Baba, amejaa neema na kweli (Yohana 1:14). Mwana wa milele wa Mungu alikuja kwetu. Ijapokuwa umaskini wetu, dhambi zetu na ujinga wetu, Mfalme wa Wafalme alikuja kufanya makao yake ndani yetu. Ninavutiwa na kutembelewa na malaika nyingi zinazozunguka kuzaliwa kwa Yesu Bwana wetu. Malaika ni wajumbe wenye nguvu, waliotumwa kutoka kwa Mungu kufanya mapenzi yake na kuwasiliana na watu. Mara nyingi katika hadithi za Krismasi, jambo la kwanza ambalo malaika anapaswa kusema ni "Usiogope."
Ni viumbe vyenye nguvu, vya kutisha vilivyotumwa kutoka mbinguni hadi duniani ili kuwasiliana na watu. Hata hivyo, malaika wa Bwana alipozungumza na Yusufu katika ndoto, ujumbe wake haukuwa wa kuogopesha, ulikuwa umejaa matumaini na amani. Malaika alimnukuu nabii Isaya akisema, “Bikira atachukua mimba na kuzaa mwana, nao watamwita Imanueli” (maana yake “Mungu pamoja nasi”) Hiyo ni kweli, malaika alimwambia Yusufu kwamba bikira ambaye alikuwa ameposwa naye angechukua mimba kutoka kwa Roho Mtakatifu na kumzaa Mwana ambaye angekuwa Imanueli, Mungu pamoja nasi. Ingawa haikutarajiwa na isiyo ya kawaida sana, habari ambazo malaika wa Bwana alimpa Yusufu zilikuwa Habari Njema kweli. Katika bustani, mwanamume na mwanamke walikuwa wameishi katika ushirika na Mungu. Lakini baba zetu walimwasi, wakaukataa wema wake.
Biblia inasema kila mmoja amepotoka. Kama kondoo, katika uasi wetu tumepotea kutoka kwa Mungu. Matokeo yake ni kuvunjika na hofu, hatia na aibu. Lakini Mungu alichukua mambo mikononi mwake. Alitutumia Yesu, Imanueli, Mungu pamoja nasi. Yesu “alijifanya si kitu kwa kuutwaa utu wa mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu (Wafilipi 2:7). Alikuja kwa walio wake, lakini walio wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake (Yohana 1:11, 12). Inashangaza! Kaka na dada, huu ndio upendo wa Mungu kwetu. Mungu alikuja kwetu katika nafsi ya Yesu. Si kwa sababu tulikuwa wema au tuliostahili, si kwa sababu tulikuwa na hekima au utajiri wa kumtolea Yeye. Hapana! Mungu alitujia sisi katika utu wa Yesu kwa sababu anatupenda.
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Kwa maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. ( Yohana 3:16, 17 ). Habari Njema hii ya Krismasi na ipenye kwa kina ndani ya mawazo na maombi yako katika siku hizi. Baba anakupenda sana. Mungu anataka kuwa nawe. Ijapokuwa makosa na uasi wako wote, ujinga wako au kiburi chako, Mungu anakupenda na amekuja kuwa nawe. Haleluya! Mwokozi gani! Yeye ni Imanueli, Mungu pamoja nasi!
Ilikuwa ''ongezeka'' na mimi Dean Davis, nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni